MIELEKEO YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU NA CHA NNE KUHUSU METHALI KINZANI: UCHUNGUZI KATIKA SHULE ZA UPILI KATIKA KATA YA TOWNSHIP, KAUNTI YA KITUI; KENYA.

Journal Title: International Journal of Advanced Research (IJAR) - Year 2018, Vol 6, Issue 10

Abstract

Ukinzani ni dhana ambayo imefasiliwa kama ubishi au upinzani. Ukinzani katika methali za Kiswahili unaweza kufasiliwa kama unyume wa kimaana unaoletwa na methali ambazo ziko katika jozi moja na zinazotoa maana zilizo kinyume. Methali za Kiswahili zina maana na ili maana hiyo ijitokeze kwa namna inayofaa, kila methali inapaswa kutumika katika mazingira yanayooana na maana ya methali mahususi. Methali zina jukumu la kuonya, kusifu, kukashifu, kuelekeza, kuliwaza na kadhalika. Aidha, katika fasihi ya Kiswahili kuna jozi za methali zilizo na maana kinyume. Kwamba, methali moja inakuelekeza huku na nyingine inakupa mwelekeo unaotofautina na ule wa awali. Katika hali kama hii, mtumiaji lugha na mwanajamii kwa jumla anaweza kupatwa na utata wa mwelekeo atakaoufuata. Methali zinapotoa maana zinazopingana basi utata unaweza kujitokeza haswa ukimsemea nwanajamii methali kisha naye akutajia iliyo na maana kinyume, huenda suluhu ya mnachozungumzia ikakosekana. Hali hii ndiyo ilimsukuma mtafiti akitaka kubainisha namna wanajamii wanavyochukulia kuwepo kwa ubishi katika methali za Kiswahili, ikizingatiwa kwamba methali hizi hutumika kila mara na wanajamii katika mazungumzo, nyimbo na hata katika uandishi.

Authors and Affiliations

Mbusya Mutei Catherine, Chomba Esther

Keywords

Related Articles

TRANSFORMATION OF NATURAL ANALCIME AND PHILLIPSITE DURING THEIR HYDROTHERMAL RECRYSTALLIZATION INTO ZEOLITES A AND X.

The objective of the present work was to study transformation of Georgian natural zeolites, analcime and phillipsite, during their recrystallization in the aim to obtain zeolites A and X, widely used for adsorption, sepa...

TAFEL POLARIZATION AND IMPEDANCE STUDIES OF AL-7075 ALLOY AND ITS COMPOSITES IN DIFFERENT MEDIUM

Aluminum metal matrix composites because of their high potential in satisfying the recent demands have a wide variety of applications in aviation, defense system, and automobile industries. It has been noticed in researc...

APPLICATION OF MALDI- TOF MS TECHNOLOGY TO THE IDENTIFICATION AND CHARACTERIZATION OF PATHOGENS IN DAIRY INDUSTRY.

The prerequisite of any microbial identiļ¬cation technique, especially in food industry, is its accuracy. Furthermore, it should be easy to perform, fast and cost-effective to ensure safe products and identify their micro...

JUSTIFICATION OF LOOK EAST POLICY AND BANGLADESH.

More than 85 Percent of Bangladesh?s export goes to the west which may seriously affect the economy of Bangladesh. The objectives are to identify the development of trade relationship with east and south Asian countries...

EXTREME WATER CONFINEMENT AMIDST SUPERHYDROPHILIC SU8 MICROPATTERNED WALLS

Control of motion of drops on solid surfaces and their mechanism is relevant in many nanotechnology processes and water vapour harvesting practices. Biomimetic strategies comprise designing topographic and chemical heter...

Download PDF file
  • EP ID EP410319
  • DOI 10.21474/IJAR01/7945
  • Views 42
  • Downloads 0

How To Cite

Mbusya Mutei Catherine, Chomba Esther (2018). MIELEKEO YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU NA CHA NNE KUHUSU METHALI KINZANI: UCHUNGUZI KATIKA SHULE ZA UPILI KATIKA KATA YA TOWNSHIP, KAUNTI YA KITUI; KENYA.. International Journal of Advanced Research (IJAR), 6(10), 1374-1381. https://europub.co.uk./articles/-A-410319